To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, May 30, 2011

Happy birthday Georgina "Shaat"

Siku ya leo alizaliwa Georgina Peter "Shaat Ole Saibul". Enjoy ur day Georgina!

Taste of Zanzibar

Kutoka kushoto ni Frank Kambira, Dr Tage Biswalo na Mukurasi Kaijage "Muki"

Thursday, May 26, 2011

FOREST HILL REUNION BEACH PARTY

YOU ARE ALL INVITED @ MBALAMWEZI BEACH CLUB ON THE 28TH OF MAY TO A FOREST HILL REUNION BEACH PARTY FROM 8pm TILL DOWN.

COME AND WATCH THE MAN U/BARCA FINALS ON THE BIG SCREEN COMPLETE WITH SOROUNDING AFTERWARDS Dj Rico WILL TAKE U DOWN MEMORY LANE TO THE DAYS OF THE REAL FOREST HILLERS.

CASH BAR WILL BE OPEN. ALL THIS FOR ONLY 7Gs

Happy birthday Mshigeni!

Mshigeni Jandwa

Happy belated birthday Irene!

Irene Meena

Happy belated birthday Beatrice

Beatrice Marco "LY 1990"

Friday, May 20, 2011

American Idol Censors Lady Gaga’s Shoes

Lady Gaga’s shoes have always been crazy, but the pair she wore to give advice to the final four contestants on American Idol this week were downright … well, they looked like penises. The $4,500 leather and Lucite platforms Gaga wore to dole out advice to James, Haley, Scott and Alaina were supported by heels that so resembled male genetalia they had to be censored on television. Gaga got the shoes from British label Void of Course, which makes lots of clothing that, well, let’s just say you’d have to be pretty creative to make any of its stuff look appropriate at your office.
The shoes are part of the label’s Impossibility of Love collection, and while we can’t say we love the shoes, we also can’t say they weren’t a provocative choice. There’s a video of Gaga’s mentorship below, and a photo of the heels right after that.

Happy birthday Winnie!

Winnie Mlahagwa Mduma anazaliwa leo usiku. Happy birthday Winnie!

Thursday, May 19, 2011

CHUO SASA KIKO WAZI NENDENI MKASOMEE KUPAMBA MAHARUSI!!

Maza Sinare
Chuo cha Maznat Vocation Training centre kilichopo Mikocheni B karibu na kanisa la mama Rwakatare nyuma ya redio Clouds kimefunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuwakomboa wanamitindo wa Tanzania pamoja na wajasiriamali wa saloon.Mkurugenzi wa Maznat Vocation centre Maza Sinare amesema chuo kinatoa mafunzo ya kutengeneza kucha, nywele, ngozi na kupamba maharusi pia wanatoa mafunzo ya kiingereza bure ili kuweza kukabiliana na soko la Afrika mashariki linalokuja kwa kasi.Chuo hicho kitatoa mafunzo kwa ngazi ya Cheti (Certificate) na bei zake ni poa na za kizalendo. Maza Sinare ameamua kuanzisha chuo hicho ili kuwakomboa wajasiriamali ambao wengi wao ni wanamitindo baada ya kutembea na kujifunza mengi ktk nchi nyingi za Ulaya na Afrika ya Kusini.

Fideline a.k.a Lady Gaga

Fideline Iranga kwenye pozi

Happy birthday Nora!

Leo Nora Hiza-Mbwile anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,kwenye picha Nora akiwa na husband wake. Enjoy ur day Sis!

Wednesday, May 18, 2011

Happy birthday Msafiri!

Leo ni siku ya kuzaliwa Msafiri Mhehe. Happy birthday Msafiri!

Happy birthday Tumaini!

Leo ni siku ya kuzaliwa Tumaini Mhehe, Happy birthday Tumaini!

Tuesday, May 17, 2011

Five Day Workshops to Prepare Students for University Life

RAIDA HIGH SCHOOL P. O. BOX 35128 TELEPHONE: +255 22 2807605  EMAIL: Raida_high@yahoo.com www.raidahighschool.sc.tz
Five Day Workshops to Prepare Students for University Life

Venue:            RAIDA High School and Learning Center
Time :              6th June – 11th June 2011
20th June  – 25th June 2011
July 11th -16th 2011

RAIDA High School and Learning Center is organising a series of workshops  targetting individuals who are entering University or tertiary education for the first time.
Purpose :  The purpose is to support first year students to manage challenges of the transition from a very protected environment of high school to an independent life and its challenges.
Some of the topics will include:
·         Setting your learning goals
·         Time management
·         Balancing social life and academics
·         Managing peer pressure
·         Stress management
·         Nurturing your spritual, mental and physical health
Mode  of Delivery
Each topic will be facilitated by experienced facilitators who will use animation and participatory approaches .
Program cost : 50, 000 Tshs only
For more details: call us at these numbers : 0786 122471, or 0688425652, 0754 82824723, 0784 622235

Monday, May 16, 2011

Taarifa ya msiba

Wana-Mlimani wenzetu David, Joseph na wengine " The Kanumba's" wamefiwa na mama yao mpendwa jana.

Poleni sana familia ya Dr. Kanumba kwa msiba huu mzito wa kuondokewa na mama yetu, tulimpenda sana lakini Mungu kampenda zaidi, jina lake lihimidiwe.

Amen

NB: Mwenye taarifa zaidi tafadhali tupeane kupitia kwenye comments.

Happy Belated birthday Paul!

Happy belated birthday Paul Meela!

SHUKRANIFamilia ya Marehemu Dr. Fanuel Christopher Shechambo wa Magamba- Lushoto inatoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki katika kumuuguza na hatimaye kutufariji katika msiba wa marehemu baba yetu mpendwa Dr. Fanuel Christopher Shechambo aliyefariki dunia tarehe 16-04-2011 huko Lushoto Tanga na kuzikwa tarehe 19-04-2011 huko kijijini Mlalo-Dule.
Shukrani za pekee tunazitoa kwa Askofu Stephen Munga na uongozi wa KKKT Dayosis ya Kaskazini Mashariki, Mkuu wa chuo Kikuu kishiriki cha Sebasitian Kolowa na wanajumuiya wote wa chuo, Chuo Kikuu cha Tumaini, Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Wilaya Lushoto, Hospitali ya Bumbuli, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), CCM Wilaya ya Lushoto, CHADEMA na CUF, Wabunge wote wa majimbo ya Lshoto, Manispaa ya Ilala, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), KKKT Usharika wa Mlalo, KKKT sharika za Tiku-Lukozi na Magamba, Kanisa la CCT-UDSM, Madrasa ya Mazizini-Lukozi, Majirani wa Dar-es-Salaam, Lushoto na Mlalo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Hongera Maza Sinare "LY 1991"!

Maza Sinare "Maznat"
Maza akila kiapoTuesday, May 10, 2011

Happy Birthday Leo!

Siku kama ya leo 10th May alizaliwa mwenzetu Leo Gwamaka "Leo The Saint". Hongera kaka!

Wednesday, May 4, 2011

Ugaidi Wa Kimataifa; Kutoka Carlos Hadi Osama Bin Laden

Na Maggid Mjengwa,

SEPTEMBA 11 mwaka huu ulimwengu utaadhimisha miaka kumi tangu kutokea kwa shambulizi kubwa la kigaidi nchini Marekani. Hakika, tangu hapo, hofu ya kutokea matukio ya ugaidi imeongezeka duniani. Na ajabu ya matukio ya ugaidi, kihistoria, mengi ya matukio makubwa ya ugaidi humu duniani yamefanyika katika mwezi wa Septemba. Kwanini?

Ni ukweli wa kihistoria, kuwa mwezi Septemba ni mwezi wenye kuambatana sana na matukio ya kigaidi. Mfululizo wa simulizi hii utakupa wewe msomaji, mwanga na maarifa juu ya mambo ambayo hukuyajua juu ya ugaidi wa kimataifa, aidha, utakupa nafasi wewe msomaji uliyefahamu kabla kukumbuka juu ya kile ulichokijua kabla.

Kupitia simulizi hii utapata pia kufahamu na kuona juu ya mahusiano ya mwezi Septemba na ugaidi wa Kimataifa. Juu ya hapo, ni imani yangu kuwa simulizi hii itakufanya uburudike na kufurahia kusoma.

Naam, Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi wa kimataifa kwa kuangalia chimbuko lake kihistoria. Katika kulifanya hilo nitatoa mifano mbalimbali.

Ni rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka 2001 kule nchini Marekani. Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu. Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam. Ilikuwa ni Agosti 7, 1998.

Sura ya ugaidi wa kimataifa imeonekana vema zaidi miongoni mwa walimwengu. Bila shaka, picha ya filamu ya televisheni yenye kuonesha majengo mawili ya World Trade Centre kule Marekani yakitunguliwa na kuanguka, zimeonwa na takribani asilimia 75 ya watu wa ulimwengu huu. Katika hili la kuchambua ugaidi, hebu basi tuanze na kujiuliza;

Ugaidi ni nini?

Itakumbukwa, kuwa mwaka 2003 wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikutana Dodoma na kupitisha Muswaada wa Ugaidi. Waheshimiwa wabunge wale walitumia muda mwingi sana kujadili tafsiri ya neno "ugaidi".

Kwa kifupi, ugaidi ukitafsiri kutoka neno la Kiingereza "Terrorism" tunapata maana ya "hofu". Neno la Kiingereza "Terror" lina maana ya hali ya "kutisha". Vitendo vya kigaidi hutumiwa na mtu au makundi ya watu ili kuwaingizia watu hofu ndani ya mioyo yao na pengine hata kuchukua madaraka ya kisiasa. Ugaidi ni njia ya mnyonge na hata mwenye nguvu kutimiza malengo yake. Hili litafafanulika zaidi kadri utakapofuatilia maandiko haya.

Kihistoria tunaona kuwa, vitendo vingi vya kigaidi humu duniani vimefanywa pia na dola zilizo madarakani kwa minajili ya kuendelea kushika hatamu za dola. Mathalan, msemo wa " Utawala dhalimu" kwa tafsiri ya Kiingereza "Terror regime" hutumika tunapoielezea dola yenye kutumia mabavu na nguvu nyingi kupita kiasi. Dola au mtawala asiyezingatia sheria wala haki za kibinadamu.

Msamiati huu wa utawala dhalimu unatokana na lugha ya Kifaransa na una chimbuko la Mapinduzi ya Wananchi kule Ufaransa kati ya mwaka 1789 hadi 1799. Utawala dhalimu wenye kutisha" la terreur" ulikuwapo kule Ufaransa kunako miaka ya kati ya 1792 hadi 1794. Katika kipindi hicho watu takribani 40,000 wengi wao wakiwa wakulima na wahunzi waliuawa.

Mifano ya tawala dhalimu na za kutisha katika sehemu nyingine za dunia ni kama Urusi ya zamani chini ya dikteta Stalin, utawala wa Kinazi wa Ujerumani kati ya 1933-1945 chini ya Fashisti Hittler. Katika Afrika, tuna pia mifano kadhaa ya tawala dhalimu na za kutisha, tawala ambazo kimsingi ni za kigaidi. Uganda ya Idi Amin, Afrika ya Kati ya Bokassa, Zaire ya Mobutu ni kati ya mifano michache miongoni mwa mingi.

Ugaidi kimsingi ni ile hali ya mtu, kikundi au dola kwa maana ya taifa kutumia nguvu nje ya wigo wa sheria ili kufikia malengo yao. Mwenye kuendesha vitendo vya kigaidi huchagua watu wake watakaoathirika na vitendo hivyo. Si lazima mtu au watu hao watakaoathirika wawe ni wahusika wa moja kwa moja wa mgogoro husika, isipokuwa waathirika mara nyingi huchaguliwa na huonekana kama wawakilishi wa malengo ambayo magaidi wanataka kuyafikia. Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.

Ugaidi huwa wa kimataifa pale tukio la kigaidi linapofanywa nje ya mipaka ya yule anayatenda tendo la kigaidi, au raia wa nchi moja wanapokuwa walengwa na kuathirika na tendo la kigaidi katika nchi ya tatu, mathalani magaidi kutoka Saudi Arabia wanapofanya tendo la kigaidi dhidi ya raia wa Uingereza katika nchi ya Zambia. Je, kuna makundi ya kigaidi ya aina ngapi? Simulizi hii itaendelea...

Monday, May 2, 2011

Happy Belated birthday Ruge!

Jana 1st May ilikuwa siku ya kuzaliwa Ruge Mutahaba. Hongera kaka!