Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika la Umoja baada ya kuwasili katika shule ya msingi Tandale iliyopo Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya wiki ya maadhimisho ya 66 ya Umoja wa Mataifa ambapo mashirika hayo yamejitolea kukarabati madarasa mawili ya shule hiyo.
Pichani Juu na Chini ni mafundi wakiendelea na kazi ya kukarabati sakafu za madara hayo.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Hassani Kalinga (wa pili kushoto) akimkaribisha Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen (wa pili kulia). Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale Renatus Pallu na Kulia ni Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Mbunju.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandale
Umoja ni Nguvu: Wafanyakazi wa UN na Walimu wa Shule ya msingi Tandale wakionyesha Umoja wakati wa kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment