To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, October 24, 2011

13 wajeruhiwa shambulio mjini Nairobi

Mmoja wa majeruhi wa bomu la mkono huko Nairibi Kenya
SHAMBULIO la guruneti katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, limesababisha watu 13 kujeruhiwa,mtu mmoja kati yao alijeruhiwa vibaya.
Guruneti hilo lilirushwa na mtu asiyejulikana.Mtu huyo alifika kwenye eneo hilo la burudani na mlango ulipofunguliwa alirusha guruneti na kukimbia.
” Mwanamume mmoja aligonga mlango akijifanya kama mteja na aliporuhusiwa kuingia ndani,akarusha guruneti” alisema mkuu wa polisi mjini Nairobi, Anthony Kibuchi.
Wengi wa waliojeruhiwa walikuwa na majeraha katika sehemu za mikono na miguu.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu.Majeruhi walikimbizwa katika hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta.
Shambulio hili linatokea wiki moja baada ya vikosi vya Kenya kuingia nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa al-Shabab, ambao Kenya inawashtumu kwa mashambulio na utekaji nyara wa watalii.
Al-Shabab walitishia kufanya mashambulio kutokana na hatua hiyo ya Kenya.

No comments: