Mweyekiti wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.
Mohamed Mwawipa mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mke wake kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali aliyopelekea wakatengana, lakini oktoba 4 walirejeana upya mahusiano yao mpaka kifo kilipomfika.
Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio hilo baada kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asingekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha aizo hazitoonekana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipoulizwa juu ya kukamatw kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea taarifa pindi atakapo pat taarifa kamilikutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali. |
No comments:
Post a Comment