WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amevunja ukimya na kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, huku akisisitiza kuwa sasa amechoka kukashifiwa.Alisema kuanzia sasa hatakubali kuchafuliwa jina lake na mtu yeyote au chombo chochote cha habari na atakayefanya hivyo, ajiandae kukabiliana na mkono wa sheria. Lowassa alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngarash Wilaya ya Monduli, Arusha kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, ikiwamo ya kuandaa na kuongoza mpango mkakati wa kumhujumu Rais Jakaya Kikwete. “Imetosha. Sasa nimeamua kukabiliana na yeyote atakayenichafulia jina na kunizulia mambo ya uongo. Nitatumia vyombo vya sheria na tayari nimewaelekeza mawakili wangu kufanya hivyo,” alisema, “Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa, nimeamua kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kisiasa na kisheria ambazo naamini zitatoa majibu sahihi dhidi ya wale wote walio nyuma ya ajenda hizi chafu kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawia ndani ya chama changu na kwa jamii nzima ya Watanzania ambao kwa muda mrefu wamelishwa mambo mengi ya kizushi na wakati mwingine ya hatari dhidi yangu,” alisema. Soma zaidi www.kwanzajamii.com |
Wednesday, October 19, 2011
Lowassa: Uvumilivu Sasa Basi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment