To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Thursday, October 27, 2011

Mary Nagu Azindua Kituo Cha Uwekezai Mbeya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TIC) nyanda za juu kusini mjini Mbeya.

Jengo la TIC Mkoani Mbeya

Akizindua ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkaribisha waziri  Mary Nagu alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Kiwira.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond  Mbilinyi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango.

No comments: