To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, October 19, 2011

Rais amteua Balozi Fulgence Kazaura kuwa Mkuu wa UDSM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Fulgence Kazaura kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Taarifa iliyotolewa jana, Jumanne, Oktoba 18, 2011, na Katibu Mkuu Kiongozi Phillemon Luhanjo imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja leo hii.

Balozi Kazaura alikuwa Mkuu wa Chuo hicho katika kipindi kilichopita kilichoishia Julai, mwaka huu, 2011.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

18 Oktoba, 2011


No comments: