HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe sasa ni mbaya na amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka kwa viongozi wa juu wa CHADEMA muda huu ni kwamba Zitto amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
“Ni kweli hali yake bado si ya kuridhisha na amehamishiwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU)…lakini anaendelea kuhimarika kwa kweli,” alisema kiongozi huyo wa CHADEMA Taifa.
Awali Zitto alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, na hali yake ilivyobadilika ghafla jana jioni alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.
No comments:
Post a Comment