Na Glady Sigera- MAELEZO- Dar es salaam
Wadau wa kilimo na uvuvi nchini wametakiwa kutumia maji yaliyopo kwa ufanisi ili waweze kupata mazao mengi kwa ajili ya kuwasaidia kupata mazao mengi kwa mahitaji ya Tanzania na nje nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika Mhandisi Mbogo Futakamba wakati akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kufungua mkutano wa siku tano wa wadau wa kilimo cha mpunga na ufugaji wa samaki kwa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa hali ilivyo sasa wakulima wengi wa mpunga hawawezi kutumia vyanzo vyao vya kilimo cha umwagiliaji ipasavyo kama vile kulima mpunga wakati huo huo wanafuga samaki ambao wangweza kuwa saidia kama chakula na kuuza kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini.
Naibu Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa mkutano huo unaozishirikisha nchi mbalimbali unaandaa mikakati itakayomsaidia mkulima kulima na kufuga samaki kwa wakati mmoja kama sehemu kuongeza uzalishaji nchini wa mazao ya mpunga na uvuvi kwa wakati mmoja.
Alisemakuwa kilimo cha aina ndio kinaweza kuwasaidia wakulima wampunga nchini na wale wa Afrika mashariki kuondokana na upungufu wa chakula na samaki.
Hata hivyo Mhandisi Futakamba alisema kuwa jumla ya bilioni 500 zinahitajika kila mwaka ili kuwezesha kilimo cha hekta laki tano (500,000) za mpunga ili kuhakikisha kunakuwepo na uzalishaji wa kutosha.
Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Tanzania ,Shirika la Kilimo na Mazao la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Misaada la Japan(JICA) .
No comments:
Post a Comment