Bodi Utalii Tanzania (TTB) ikishirikiana na kampuni mbalimbali za Utalii imeshiriki maonesho ya Utalii yaliofanyika nchini Uingereza yajulikanayo kama World Travel Market kuanzia tarehe 7-10, 2011. Jumla ya kampuni 62 kutoka Tanzania bara na visiwani walishirikia maonesho haya na Waziri wa Maliasili ya Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mheshimiwa Abdillah Jihad Hassan viongozi wa wa serikali waliohudhuria maonesho haya. Katika maonesho haya Banda la Tanzania lilikuwa kati ya mabada makubwa kwa upande wa Afrika na lilikuwa na picha zinazoonesha vivutio vya Utalii vya Tanzania vilevile kulikuwepo bango kubwa linalohasisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Banda la Tanzania lilivyooneka wakati wa maonesho yaliofanyika nchini Uingereza tarehe 7-10 Nov 2011. |
No comments:
Post a Comment