To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, January 18, 2012

JK Ziarani Morogoro



Rais Kikwete na ujumbe wake na wenyeji wakipita juu ya daraja jipya la  Mtombozi, Matombo, Morogoro vijijini alilozindua leo. Rais Jakaya Kikwete leo ametembelea Morogoro vijijini na kuzindua madaraja mawili makubwa katika mto Mtombozi, Matombo, na mto Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, pia ameweka jiwe la msingi la soko la kijiji cha Mtamba na kukagua ujenzi wa barabara sehemu ya Kisaki, Msalabani.

Rais Kikwete akielekea jukwaani kuhutubia wananchi  baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kijiji cha Mtamba, Morogoro vijijini.

Rais Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera (shoto) akivuka daraja jipya la Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, Morogoro Vijijini baada ya kulizindua.

Rais Kikwete akiongea na baadhi ya wananchi baada ya kuzindua daraja la mto Mtombozi tarafa ya Matombo wilaya ya Morogoro mjini leo January 17, 2012

No comments: