To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, January 16, 2012

Marehemu Rejia Mtema kuagwa Januari 17

Marehemu Mbunge Rejia Mtema

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini (kushoto) akichukua maelezo kwenye gari la Regia Mtema namba T296 BSM baada ya ajali.

Gari la Mbunge Rejia Mtema baada ya ajali

Mbunge wa CHADEMA, Rejia Mtema aliyefariki juzi kwa ajali ya gari anatarajiwa kuagwa kesho Januari 17 jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea Ifakara mkoani Morogoro kwa mazishi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika (Mb) imeeleza kuwa heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa, Januari 17, 2012.

Mnyika amesema baada ya kuagwa, marehemu atasafirishwa mpaka Ifakara ambapo maziko yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Januari 18, 2012.
“CHADEMA tunaendelea kujumuika na familia ya Regia Mtema, bunge na wapenda demokrasia na maendeleo wote nyumbani kwa baba wa marehemu, eneo la Tabata Chang’ombe. Marehemu Regia Mtema ni nyota iliyotoweka mapema lakini kumbukumbu yake itaendelea kuwepo kwa chama na kwa taifa,” amesema katika taarifa hiyo.
Marehemu Regia Estelatus Mtema aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira, alifariki jana papo hapo eneo la Ruvu Darajani baada ya gari lake aina ya Toyota VX kumshinda na kupinduka.

No comments: