To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, March 6, 2012

Dr. Kawambwa Atembelea Ardhi University (ARU)

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) akifafanua jambo wakati wa akijibu maswali kutoka kwa watumishi na wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kufanya ziara katika Chuo Kikuu Ardhi Dar es Salaam kwa ziara ya Mafunzo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro na aliekaa kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala Prof. Eliutha Mwageni.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro, (kulia) Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala Prof. Eliutha Mwageni (Kushoto ) na baadhi ya watumishi wa Chuo Kikuu Ardhi. Picha zote na Hadija Maulid na Mary Kigosi wa Chuo Kikuu Ardhi.

Dk Evaristo Liwa, Mkuu wa Kitengo cha Geospatial Science katika Chuo Kikuu Ardhi akimwonesha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) mitambo mbalimbali inayotumika kufundishia wanafunzi chuoni hapo. Kushoto ni Makamu Mkuu Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro.

Makamu Mkuu Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akimweleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) mitambo mbalimbali inayotumika kutengeneza Ramani za miji kupitia picha za anga na satellite. Waziri Kawambwa alifanya ziara ya mafunzo chuoni hapo jana kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za Chuo hicho.

No comments: