To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, March 14, 2012

Vifaa Vya Kisasa Vya Kuzimia Moto Vyazinduliwa Dar

Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi akimwelekeza katibu mkuu Mbarak Abdulwakil katikati jinsi ya kuuweka ufunguo wa kifaa hicho kabla ya kukirusha ndani ya kontena lenye moto, Kushoto ni Damian George Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil kushoto akipokelewa na Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited na makamanda wa kikosi cha Zima moto, mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio tayari kwa uzinduzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil kulia akipokea moja ya vifaa hivyo DSPA 5 kutoka kwa Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini , wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa kikosi cha Zimamoto Kamanda Pius Nyambacha na anayefuatia ni Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil katikati akiongozana na Damian George Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini kuelekea katika eneo la uzinduzi, kulia ni Kamishna wa kikosi cha Zimamoto Kamanda Pius Nyambacha.

Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi akiwaelezea wageni waalikwa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Mbarak Abdulwakil pamoja na Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi inayotengeneza vifaa vya kuzimia moto vyenye teknolojia ya kisasa vinavyoitwa DSPA 5, wakikiandaa kifaa hicho kwa ajili ya kukirusha ndani ya kontena lililowashwa moto, ili kufunga mlango na kuruhusu kifaa hicho kufungua gesi ya Oxgen baada ya sekunde sita tayari kuzima moto huo ndani ya kontena hilo, tukio hilo lilikuwa ni uzinduzi wa vifaa hivyo hapa nchini, uliofanyika katika viwanja vya Kikosi cha kuzima moto Fire jijini Dar es salaam leo.

Askari wa Kikosi cha kuzima mto wakiwa tayari kwa kuimza masalia madogo madogo ya moto baada ya kifaa hicho kufanya kazi yake kikamilifu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil pamoja na viongozi wa kampuni hiyo na wakuu wa kikosi cha kuzima moto wakishuhudia moshi mkubwa ukitoka kwenye kontena hilo baada ya kifaa hicho kuanza kazi yake ya kuzima moto.

No comments: