To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, January 18, 2011

Halima Mdee a.k.a Kamanda "LY 1991" - Mbunge kijana anayepigania kurejeshwa kwa hadhi ya Bunge

Mheshimiwa Halima Mdee (Mb)
 Halima James Mdee "LY 1991" alizaliwa Machi 18, 1978 katika Kijiji cha Makanya, Wilaya ya Moshi Vijijini, ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya Msingi Mlimani.

Halima alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.

Mwaka 1996 hadi 1998 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro na 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea sheria na kuhitimu mwaka 2003.

Aliajiriwa na Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana mwaka 2004 akiwa Ofisa Maendeleo kama mwanasheria mpaka mwaka 2005 alipoamua kuacha kazi na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu, ambako alishiriki kuwapigia kampeni wagombea wa CHADEMA kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.

Halima alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa na kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima.
Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki kama shukurani kwa kanisa kutokana na msaada mkubwa lilitoa kwa familia hiyo ambao Halima alikataa kuueleza.
Mbali na ubunge, pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la CHADEMA, na ofisa katika kurugenzi ya sheria.

No comments: