To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Sunday, October 23, 2011

Arusha Yatamba Mbio Za”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge 2011"

Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli  Mkoa wa Mwanza na Shinyanga Elisha Eliasi akizindua mbio za Vodacom  Mwanza Openi Cycle Challenge 2011,katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa  Serengeti Breweries Ephraim Mafuru na Meneja Mauzo wa  Vodacom  kanda ya Ziwa Amos Vuhahula,Mbio hizo zilianzia mjini Shinyanga na  kumalizikia Bugando Jijini Mwanza,Mbio hizo ziliandaliwa na Vodacom  Tanzania na kudhaminiwa na kinywaji cha Malta Guinness.


Mkurugenzi wa masokko Serengeti Breweries  Ephraim Mafuru,akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa mbio za walemavu  ambazo pia zilikuwa moja ya mbio hizo katika mbio za”Vodacom Mwaza Open  Cycle Challenge 2011 kudhaminiwa na kinywaji cha Malta Guinness.

Mshindi wa kwanza wa mbio ndefu za za baiskeli za”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge Kilometa 196  Richard Laizer (Arusha) akimaliza mbio hizo alipotumia Masaa 5:02:28  katika  mbio hizo,zilizoanzia Shinyanga na kumalizikia jijini Mwanza,Mbio hizo  ziliandaliwa na Vodacom Tanzania na kudhaminiwa na kinywaji cha Malta  Guinness.

Baadhi  ya washiriki wa mbio za baiskeli za”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge  wakichuana vikali katika mbio hizo,zilizoanzia Shinyanga na kumalizikia  jijini Mwanza,Mbio hizo ziliandaliwa na Vodacom Tanzania

Hatimaye Richard Laizer  wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha nani anayepaswa kuwa  mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza Open  Cycle Challenge  baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 400 walijitokeza kushiriki  kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanaume.Hapa mshindi huyo wa mbio za Mwanza Open Vodacom Cycle Challenge 2011 kutoka klabu ya Arusha Cycling Richard Laizer akipokea zawadi yake ya shilingi milioni 1.500.000 kutoka kwa Mkuu wa  Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mara baada ya kutajwa katika mbio hizo za kilomita 196 zilizoanzia Busanda mkoani Shinyanga na kumalizikia Bugando Hills jijini Mwanza.

kurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya  Serengeti SBL Ephraim Mafuru akikabidhi zawadi kwa Zavalina Abel aliyeshiriki katika mbio za kilomita 10.
Hatimaye  Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha nani  anayepaswa kuwa mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza  Cycle Challenge baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 400  walijitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanaume. Kutokana  na ushindi huo amejinyakulia zawadi ya shilingi Milioni Milion Moja na  Nusu na kuvikwa taji lililokuwa likishikiliwa na Hamis Clement wa  Shinyanga baada ya kutumia muda wa Masaa 5:02:28 kumaliza mbio hizo za  kilometa 196. Mshindi  wa pili wa michuano hiyo kwa wanaume ni Mindi Mwagi kutoka mkoani  Shinyanga aliyetumia saa 5:02:29 ambaye amezawadiwa shilingi Milioni  Moja akifutiwa na mshindi wa tatu Said Jumanne aliyezawadiwa kiasi cha  shilingi Laki saba yeye akiuwakilisha mkoa wa Arusha. Kwa upande wa  wanawake Mkoa wa Arusha  uliibuka  kidedea baada ya mshiriki wake Bi Sophia Hussein kuwabwaga washiriki  wenzake zaidi ya zaidi 60 na kunyakua nafasi ya kwanza katika mashindano  hayo ya kilometa 80 baada ya kutumia muda wa Masaa 2:25:13 kumaliza  mbio hizo. Hivyo kwa ushindi huo Bi Hussein amejishindia kitita cha shilingi Mil1,100,000  na kushikilia taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Sophia Adison wa  Arusha huku akifuatiwa na mshindi wa pili Bi Mwajuma Musa kutoka mkoani  Arusha aliyetumia Masaa 2:25:40 na kujinyakulia zawadi ya shilingi Laki  nane. Hata  hivyo mkoa wa Shinyanga nao haukuwa nyuma katika mashindano hayo baada  ya Bi Salome Donard baada ya kushika nafasi ya tatu ambapo alizawadiwa  kiasi cha shilingi 600,000 baada ya kutumia Masaa 2:26:21 kuhitimisha mbio hizo za kilometa 80 kwa wanawake. Akizungumza baada ya mashindano hayo,Richard Laizer alisema kilichomsadia ni mazoezi  na  maandalizi ya mara kwa mara aliyokuwa akiyafanya ingawa mlima wa  Bugando wa kumalizia mbio hizo ulimsumbua katika mashindano hayo.“Nashukuru  kwa kumaliza salama na kuwa bingwa katika michuano hii, kutokana na  zawadi hii niliyopata kutoka Vodacom Tanzania na wadhamini Wenza  Serengeti Breweries kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta  Guinness nitajiendeleza zaidi ili kufikia viwango vya uendeshaji  baiskeli kimataifa,” alisema Laizer.Kwa  upande wake Bi. Sophia Hussein alisema mashindano ya mwaka huu kwake  yalikuwa na upinzani mkali kwa sababu ushindani ulikuwa ni wa hali ya  juu hasa wenye baiskeli za Phoenix ambao walikuwa hawampi nafasi. Mkurugenzi  wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Bw Steven Kingu,ambae ndiye alikuwa  mgeni rasmi aliwapongeza washiriki wote hususani washindi na kuahidi  kwamba kampuni yake itaendelea kuratibu, kuandaa michuano hiyo ili  kuifanya kufikia michuano ya kimataifa. “Nimefarijika  kwa mbio hizi za wazi za Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge kuendelea  kuwa bora kila mwaka na hili linatupa changamoto za kuendelea kuandaa na  kudhamini katika mikoa mingine kama sio Tanzania nzima,” alisema Kingu. Kwa  upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Breweries  Limited (SBL) Ephraim Mafuru ambao ni wadhamini wenza kupitia kinywaji  kisicho na kilevi cha Malta Guinness alisema hawajutii kudhamini  michuano hiyo kutokana na hadhi iliyonayo “Tumeshuhudia  kupitia udhamini wetu washindi wamejipatia zawadi ambazo kama  watazitumia vema zinaweza kuwa mitaji itakayowawezesha kujiletea  maendeleo katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla,” alisema Mafuru.

No comments: