To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Sunday, October 23, 2011

Kariakoo kwatapakaa maji ya kinyesi!

Baadhi ya mafundi wa kuzibua chemba za maji ya vinyesi wa Kampuni ya DAWASCO wakiangaika kuyazuia maji ya vinyesi kuendelea kutiririka katika mitaa mbalimbali ya Soko la Kariakoo baada ya chemba hizo kuziba na maji kutiririka hovyo

Baadhi ya wananchi wakipita kwa tabu katika mitaa iliyokuwa ikitiririka maji ya vinyesi leo Dar es Salaam hivyo kuwa kero kubwa kwao kutokana na harufu mbaya kuenea maeneo hayo.
Baada ya maji hayo kutiririka kwa muda mrefu majira ya mchana walifika wafanyakazi wa kampuni ya DAWASCO huku wakiwa na gari maalumu la kuzibulia chemba za maji taka. Hata hivyo walishindwa kuyadhibiti maji hayo na kuendelea kutapakaa huku yakikanyagwa na baadhi ya wapitanjia maeneo hayo jambo ambalo lilikuwa hatari kiafya. Baadhi ya wapitanjia walisikika wakisema; “Kweli hili jiji (Dar es Salaam) limewashinda viongozi wahusika hivyo kuna haja ya kutafuta watu kutoka nje labda wanaweza kuleta mabadiliko…haiwezekani kila wakati miundombinu ya maji taka ikawa kero namna hii tena kwenye jiji maarufu kama hili.”
Hata hivyo juhudi za Thehabari.com kuwapata viongozi wa soko kungumzia hali hiyo hazikuzaa matunda hadi mwandishi anaondoka eneo la tukio.

No comments: