To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, October 25, 2011

Kilele Cha Wiki Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje Jijini Dar es salaam

Waziri Membe akisalimiana na wawakilishi wa mbalimbali wa Umoja wa Mataifa mara baada ya kuwasili.

Bendi ya Shule ya Sekondari Jitegemee ikitoa burudani mbele ya wageni waalikwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri Membe akikagua gwaride

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe, akihutubia katika sherehe za kilelel cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na miaka 66 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Membe aliishukuru UN kwa msaada mkubwa inaoupatia Tanzania kupitia wakala wake wa maendeleo na kusisitiza kuendeleza mema yote na kutatua changamoto  zinazoikabili nchini hususani katika ongezeko la watu Duniani ambalo linatarajiwa kufikia Bilioni 7  mwaka huu na uwepo wa changamoto nyingi na nafasi mbalimbali

Wawakilishi kutoka Balozi mbalimbali na viongozi wa Serikali wakifuatilia sherehe hizo zilizokuwa zikendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Maafisa mbalimbali wa Majeshi nchini wakitoa heshima wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na 66 ya Umoja wa Mataifa iliyoenda sambamba na ufungaji wa wiki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou akisoma hotuba wakati wa maadhimisho ya Miaka 66 ya Umoja wa Mataifa iliyoenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Mwakilishi Mkazi huyo aliisifu nchi ya Tanzania kwa kuendeleza Amani na Uutulivu vilivyoachwa na Mwasisi wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ambapo alisihi kuwepo kwa  uangalizi wa karibu katika masuala ya Kijamii  na changamoto zinazoikabili nchi katika kipindi hichi cha kuyumba kwa Uchumi na matatizo ya Kisiasa.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini, Fancy Nkuhi, akisoma Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban-Ki Moon katika maadhimisho ya 66 ya UN yanayoenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Nkuhi ameelezea Kusikitishwa kwake na matukio ya udhalilishwaji wa Wanawake, vifo vya Wanawake vinavyotokana na migogoro ya ndani, tabia ya Ukeketaji wa Watoto wa Kike akitolea mfano tukio la hivi Karibuni la Kukeketwa  kwa mtoto wa Mwaka mmoja na muhusika bila kuchukuliwa hatua, pamoja na kuozeshwa kwa mabinti wadogo bila ridhaa yao.

No comments: