To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Sunday, October 9, 2011

Mabalozi Watembelea Kaburi La Mwalimu Nyerere, Mwitongo Butiama

Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa akitoa maelekezo kwa  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe wakati wa ziara ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa waliotembelea leo makazi na kaburi na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kijijini kwake Butiama mkoani Mara.

Mama Maria Nyerere akiwa kwenye picha ya pamoja na mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa wakati walipotembelea kaburi na makazi ya Hayati Baba Mwalimu Julius Nyerere katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. Waliokaaa kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mabalozi, Balozi Juma Mpango, anayemfuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa, pamoja na Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe. Kulia ni motto wa Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.


Baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa yaliyopo nchini wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe wakati walipotembelea kaburi na makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kijiji Butiama, mkoani Mara

Mama Maria Nyerere( katikati) akiwa na Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini Balozi Juma wakiomba dua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kijijini Butiama wakati mabalozi hao walitembelea makazi na kaburi la Mwasisi huyo wa taifa la Tanzania. Wengine katika picha wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe wakati kwa upande wa kulia ni mwanae Charles Makongoro Nyerere.

No comments: