Kiapo hicho kimeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania m Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri na maafisa wengine serikalini.
Mara baada ya kula kiapo hicho, Rais Wa Zanzibar amehudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Kikwete. Mara baada ya Baraza la Mawaziri kukamilika jioni leo, Rais anatarajiwa kuelekea Perth Australia kuhudhuria kikao cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kinachofanyika kuanzia tarehe 28-30 mwezi huu.
Kabla ya Mkutano mkuu kuanza, tarehe 25 October, kutakua na vikao kadhaa kikiwemo kikao cha wafanyabiashara ambacho Rais Kikwete anatarajiwa kutoa hotuba ya ufunguzi na baadae kujumuika na viongozi kadhaa wa nchi chache katika kikao maalum na wafanyabiashara.
Rais anatarajiwa kurejea nchini tarehe 1 Novemba, 2011. Mapema leo asubuhi Rais amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi kutoka Sudan na Japan. Balozi Mteule wa Sudan Yassir Mohamed Ali amewakilisha hati zake kwanza na kufuatiwa na balozi Masaki Okada.
No comments:
Post a Comment