Chadema mkoa wa Dar es salaam wanaandamana kesho kupinga kudhalilishwa kwa viongozi wake, wabunge na wanachama wake huko Arusha na Matatizo mengi yanayoikumba nchi.Hayo yamesemwa na ndugu John Heche Mwenyekiti wa BAVICHA taifa aliyesoma taarifa kwa vyombo vya habari(pichani kulia),akisaidiana na Mwita Mwikwabe mkurugenzi wa sera na utafiti(kulia haonekani kwenye picha).Heche amekanusha taarifa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa mh Mbowe amekimbia kusikojulikana.Amesema yupo Arusha na chama hakitahangaika kumuwekea dhamana,kwani kufanya hivyo nikuingia kwenye mtego wa CCM na washirika wao.Alipoulizwa ikiwa polisi wameruhusu maandamano yao hapo kesho, Mwita alirejea sheria ya vyama vya siasa akisema haitaji kuomba kibali bali kutoa taarifa ndani ya saa 48 jambo ambalo limeshafanyika.Ameongeza kuwa hata kama polisi watakuja na visingizio vya al shabaab bado wao wataendelea na maandamano kama walivyopanga.Kesho saa tatu asubuhi kuanzia kimara kwenye ofisi za Chadema hadi Manzese Bakhresa.Ameongeza kuwa maamuzi ya maandamano yataishaje na wapi yatategemea hali ya ushirikiano wa polisi. |
No comments:
Post a Comment