To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, November 2, 2011

Miss Tanzania aingia 16 bora ya Beauty with Purpose

Miss Tanzania 2011, Salha Israel amefanikiwa kuingia nusu fainali ya taji la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) yaliyofanyika juzi nchini Uingereza.
Akizungumza kutoka London jana, Salha alisema kuwa katika taji hilo, mrembo huyo aliwasilisha kazi yake ya Jamii aliyoifanya kwenye hospitali ya Muhimbili ambako alisaidia watoto wenye matatizo ambao wanazaliwa chini ya mwezi moja.
Salha alisema kuwa katika shindano hilo, Salha aliwakilisha DVD inayonyesha jinsi gani alivyomsaidia mtoto aliyezaliwa kwenye hospitali hiyo huku akiwa na kidonda kikubwa mgongoni.
“Haikuwa kazi rahisi kwa majaji wa shindano hilo kuona ninavyofanya kazi ya kumsaidia mtoto huyo, ni kazi ambayo imewafanya waikubali kwani ipo katika majukumu ya Kamati ya Miss World mbali ya shindano lenyewe la urembo,” alisema Salha kwa njia ya simu.
Alisema kuwa amefarijika kuingia katika hatua hiyo ya 16 bora katika shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya warembo 122 kutoka nchi mbali mbali.
“Ninachokisubiri sasa ni fainali ya taji hili ambapo mshindi ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo itashirikisha si chini ya warembo 20,” alisema.
Kuhusiana na mashindano, Salha alisema kuwa mashindano ni magumu ukilinganisha na mashindano ya Miss Tanzania kutokana na mambo makubwa moja.
Alisema kuwa sababu hiyo ni idadi ya washiriki ambao ni wengi ukilinganisha na warembo 30 wanaoshiriki Miss Tanzania na vile vile wapo bora zaidi kulinganisha na mashindano ya kitaifa.
“Ninawaomba Watanzania ni waniombee ili niweze kufanya vyema katika mashindano, ni magumu kwa kweli,” alisema.
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim "Uncle" Lundenga alimpongeza Salha kwa hatua hiyo na kusema japo anakabiliwa na kibarua kikubwa ili aweze kufanya vyema.
"Ni matokeo mazuri, lakini kazi bado ni kubwa, tunatakiwa kumwombea ili aweze
kufanya vyema zaidi," alisema Lundenga.

No comments: