Mkuu wa Uhusiano wa Bodi ya Utalii nchini TTB Geofrey Tengeneza akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bodi hio zilizopo katika jengo la IPS wakati akizungumzia kuupigia kura wa mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda na kuwa moja ya maajabu ya dunia kutoka barani Afrika. Tengeneza amesema imeonyesha kwamba watanzania karibu asilimia 20% tu ndiyo walioupigia kura wakati asilimia 80% iliyobaki kura zimepigwa kutoka mataifa mbalimbali Marekani. Ulaya na Afrika.
Amewahimiza watanzani kuupigia zaidi mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda na kuwa moja ya maajabu ya Dunia, watu wanaweza kupiga kura kwa kutuma ujumbe Mfupi wa Kili kwenda namba 15771 kwenda mtandao wowote wa simu hapa nchini, ameongeza kwamba pia Kampuni ya Pamoja Marketing inayofanya masoko ya utalii duniani kote ndiyo imepewa dhamana ya kuutangaza utalii wa Tanzania na kuhakikishwa kwamba mlima Kilimanjaro unatangazwa kote duniani pamoja na vivuti vingine vilivyoko nchini . |
No comments:
Post a Comment