To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Thursday, January 19, 2012

JK, SPIKA NA LOWASSA KATIKA MSIBA WA MAREHEMU JEREMIAH SUMARY

Rais Dk Jakaya Kikwete Akimpa pole mjane wa Marehemu Jeremia Sumary, Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha wa wa zamani aliyefariki leo asubuhi jijini Dar es salaam. Hapa ni nyumbani kwa marehemu, Mbezi Beach, Dar es salaam jioni hii. Picha na Ikulu

Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa Picha na Owen David

Rais Dk. Jakaya Kikwete akitoa pole kwa wafiwa.

JK akiongea na ndugu wa marehemu pamoja na Spika Anne Makinda na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa ambaye ni mzazi wa binti aliyeolewa na mtoto wa marehemu Sumary

 Rais Dk. Jakaya Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo. Picha na Ikulu

No comments: