To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, March 20, 2012

Lowassa Ahudhuria Sherehe Za Kusimikwa Askofu Melchior Libena

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi na mkewe Mama Sitti Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada ya kusimikwa uaskofu mjini Ifakara jana.

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo, Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika jana Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akizungumza na wananchi na wageni waalikwa baada ya ibadara ya kusimikwa Askofu mpya wa Jimbo la Ifakara, Salitaris Melchior Libena.

Watoto wa Utatu Mtakatifu wakicheza kwenye ibada hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiongozana na Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena jana mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika jana Ifakara, mkoani Morogoro.

No comments: