Tumepata malalamiko kutoka kwa wana-Mlimani waliokuwepo kwenye party iliyofanyika hivi karibuni kuwa tumeweka picha nyingi humu kwa upendeleo, kama mtakumbuka kwenye post ya kwanza kabisa ya blog hii tuliwaomba kama kuna yeyote ana picha za BBQ azitume kupitia watotowamlimani@gmail.com ili tuzipandishe, picha zote tulizoweka zimetumwa na watu mbalimbali ambazo walizipiga wao wenyewe na hakukuwa na mpiga picha maalum katika tukio lile hivyo bado tunaendelea kuwaomba kama mnazo picha zaidi mzitume kwa address tajwa hapo juu. Tutumie hata picha za zamani alimradi ni zako wewe au na familia yako.
Asante!
No comments:
Post a Comment