To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, February 16, 2011

Taarifa ya Msiba

Mlimani Blog inasikitika kutangaza kifo cha Profesa Chrisant Kamuzora kilichotokea juzi siku ya jumanne tarehe 15/2/2011 kwa ajali ya kuangukiwa na mti katika viwanja vya Gymkhana Club. Marehemu Prof. Chrisant Kamuzora ni baba wa wana-mlimani Mukajungu "LY 1988" na Martha "LY 1990". Msiba upo nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar na leo hii mchana saa nane kamili mwili wa marehemu utaagwa na kupewa heshima za mwisho katika ukumbi wa NKRUMAH Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kesho asubuhi tarehe 18/2/2011mwili utasafirishwa kuelekea nyumbani Bukoba kwa kuulaza kwenye nyumba ya milele.

Mlimani blog inawapa pole familia ya marehamu Prof.Kamuzora kwa msiba huu mzito na Mungu awatie nguvu na imani.

Mwanga wa milele amwangazie na apumzike kwa amani. Amen!

1 comment:

Anonymous said...

Poleni sana Martha and the whole Kamuzora clan, kazi ya mwenyezi mungu haina makosa.
R.I.P Dear Prof..mourn you till we join you.