To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Saturday, October 1, 2011

AJALI YAUA WATU 6 DODOMA YAJERUHI 23

IGP Said Mwema
MZIMU wa ajali sasa watoka Mbeya watua Dodoma baada ya watu Sita wamekufa Papo hapo na wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Pandambili Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma JOSEPH MWAKABONGA ameiambia uhuru fm kuwa kati yao waliokufa Mwanaume ni mmoja na Wanawake ni Watano.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika Kijiji hicho cha Pandambili kwenye njia Panda ya Mlali na imehusisha gari aina ya Heicher yenye namba za usajili T-415-DSK ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kwenda Dar es salaam.

Dereva wa gari hilo COSMAS SHOMARI amekimbia na Polisi inaendelea kumtafuta.

Waliokufa ni ABIJELI MBANILA, PEMBE MAKARANGA, Mtoto miaka mitatu aliyetambulika kwa jina moja la EVELINY, NORINA RICHARD, Mtoto wa miezi 10, na wengine wawili hawajatambuliwa.

Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni Dereva alikuwa anaendesha gari pembeni zaidi mwa barabara ambalo liliacha njia na kuvutwa kulia mwa barabara na kisha kupinduka katika kalavati.

Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa na wengine wamelazwa katika Zahanati ya Kibaigwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

No comments: