Juma Mwapachu |
Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Juma Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 14 Septemba 2011. Atakuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne (4)
Balozi Mwapachu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe.Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kwanza na sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.Balozi Juma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunga na Jeshi la Polisi nchini.
Mhe.Balozi Juma Mwapachu aliwahi kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.

No comments:
Post a Comment