To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, November 21, 2011

Miaka 10 Ya SUZA


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada  Rai akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari ambao hawapo pichani  katika uzinduzi wa Sherehe za kutimiza Miaka 10 ya Chuo hicho, kushotoni  kwake ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dk. Abdallah Ismail Kanduru


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada  Rai akizindua CD ya Utafiti wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Visiwa  vya Zanzibar kwa Waandishi wa Habari katika hafla iliyofanyika Chuoni  hapo Vuga Mjini Zanzibar.


Mmoja kati ya Waandishi wa Habari akiuliza Swali kwa Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai ambaye hayupo  pichani katika uzinduzi wa Sherehe za kutimiza Miaka 10 ya Chuo hicho  kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Vuga Mjini  Zanzibar.
PICHA ZOTE NA Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar

Na Khadija Khamis  – Habari Maelezo.
Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha  Taifa Zanzibar ( Suza ) Profesa Idris Ahmed  Rai amesema,   wakati umefika sasa Chuo hicho kuwa ni chuo chenye hadhi ya kimataifa  ili kiweze kutambulika duniani kote .
Aliyasema hayo leo huko katika  uzinduzi wa sherehe za miaka kumi ya Chuo Kikuu cha  Suza ambazo zinatarajia kufikia  kilele chake siku ya tarehe 24 mwezi huu.

Katika uzinduzi huo Profesa  Rai alisema kuwa, ni dhahiri kwamba kuna mengi sana zaidi ya kuyafanya  katika kukiwezesha chuo hicho kuwa ni chuo kikuu na chenye hadhi ya   kimataifa nchini .Aidha alisema kuwa wakati umefika  sasa Suza kutanua huduma zake za masomo na tafiti kwa jamii ya wazanzibari  na ulimwengu kwa ujumla pamoja na kukuza  uwiano  wa karibu sana  kati ya maendeleo ya nchi na ukuwaji wa elimu ya juu .

Akifahamisha kuwa ukuwaji wa  elimu ya juu ni changamoto kwa taifa kwani ukuwaji huu unalenga katika  kusukuma mbele maendeleo ya nchi na ukuwaji wa uchumi .nchini.
Ameeleza kuwa mpango wa  Chuo  hicho unatarajia kuwa na skuli  kadhaa ambazo zitatoa masomo na mafunzo  tofauti ambayo ni muhimu kwa jamii yetu na mahitaji ya ulimwengu wa  sayansi na teknolojia.

 Alifahamisha kuwa ukuwaji  wa chuo hicho unatarajiwa kuwa katika  awamu  tofauti ambapo katika  awamu  ya kwanza, kunatarajiwa kuanzishwa skuli ambazo zinatokana na  na idara au taasisi zilizopo hivi sasa ili kuweza kutoa fursa   muhimu kwa skuli na idara zake mpya kuwa na uwezo mkubwa wa kukuza programu  zake
 Alieleza kuwa chuo kikuu cha  suza kinajipanga vyema kuisaidia serikali katika kufanikisha sera yake  ya kukuza utalii kwa kuweza kusomesha utalii  katika chuo hicho  na skuli hiyo itaundwa kuwatayarisha vijana kuwa na ujuzi wa kazi katika  sekta hii ili waweze kunufaika kiajira.
 Akifafanua azma ya chuo hicho  Profesa Rai  alisema kuwa, ni kukifanya  chuo kua bora zaidi katika  ukanda wa  Afrika Mashariki na chenye kutoa elimu yenye kiwango  cha  hali ya juu katika vigezo vya kimataifa.



No comments: