To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, December 6, 2011

Anna Makinda Azindua Ripoti Ya Dunia Ya Umoja Wa Mataifa Kuhusu Haki, Idadi Ya Watu Na Ujana Tanzania

Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akitoa ujumbe wa umoja wa mataifa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ongezeko la idadi ya watu,masual ya wanawake na watoto leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiongea vijana na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa  waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki za watoto, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akizindua ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki za watoto nchini, idadi ya watu na masuala ya vijana akiwa ameungana na baadhi ya vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya vijana waliohudhuria uzinduzi wa ripoti  ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ya spika wa Bunge Anne Makinda ambaye alikuwa  mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi mkazi wa UNICEF nchini Tanzania Bi. Dorothy Rozga akitoa ujumbe maalum wa shirika hilo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu, Haki za watoto na masuala ya wanawake na watoto leo jijini Dar es salaam.
 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akimpongeza kijana Mohamed Kessy kutoka Mbeya mara baada ya kijana huyo kuwasilisha matamko mbalimbali  ya watoto yakiwemo uboreshaji wa elimu,utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa jamii, elimu ya maambukizi ya VVU na Ukimwi, Masuala ya ulinzi na ukatili dhidi ya watoto pamoja na sheria zinazolinda  na kutetea haki za watoto leo jijini Dar es salaam
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments: