To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, December 5, 2011

NBC Family Day 2011 Yafana

Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika kuvuta kamba ili kumpata mshindi  katika Siku ya wanafamilia ya
benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika mbio za magunia katika Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika
Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam. Robert  Kusekwa (wa pili
kulia) alibuka kidedea.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto)
akishiriki kusakata dansi lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya FM
Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia
wa benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.


Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC wakifurahi katika
bwawa la kuogelea ikiwa ni baadhi ya burudani kuadhimisha Siku ya
Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika mchezo wa kufukuza kuku katika Siku ya Wanafamilia ya benki
hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.  Mshindi wa mbio
hizo huondoka na kuku huyo na kwenda nae kumfanya kitoweo au kumfuga.

No comments: