To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, December 21, 2011

TAARIFA YA MSIBA

Kanali Mstaafu Raphael Marwa Horombe
Mlimani Blog inasikitika kutangaza kifo cha Kanali wa Jeshi Mstaafu Raphael Marwa Horombe ambaye ni baba wa wana-Mlimani wenzetu Odesa, Henry na wengineo kilichotokea mkoani Tanga kwa ajali ya gari siku ya Jumamosi usiku tarehe 17 Disemba 2011.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Dar es Salaam siku ya Jumatatu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Makongo Juu Dar es Salaam na mazishi yatafanyika kijijini kwake Tarime Mkoani Mara siku ya Jumamosi tarehe 24 Disemba 2011.

Mlimani Blog inawapa pole wafiwa wote na Mungu ailaze roho ya Marehemu Baba yetu mahali pema peponi, AMINA!

No comments: