To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Monday, December 5, 2011

Vijana Waanza Safari Kuupandisha Mlima Kilimanjaro

Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wanaonekana wakianza safari yao kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Marangu Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011. Picha na Anna Itenda -Maelezo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidas Gama akimpa mkono wa kumtakia heri mmoja wa vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro zilizoko Marangu Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama pamoja na Viongozi wa Mkaoa wa Kilimanjaro na wawakilishi wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo wakiwasindikizaVijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro tayari kwa safari leo Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro.

Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro walioagwa rasmi na Mhe.Rais Jakaya Mrisho Kikwete Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam hivi karibuni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akiwaaga kwenye shughuli fupi iliyofanyika Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011

Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa tayari kwa kuanzakupandisha mlima huo na Mwenge.

No comments: