To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Sunday, December 4, 2011

Vodacom Yazindua Kampeni Ya Share and Care

 Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Stela Chiwango akimkabidhi mbuzi mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo kimara jijini Dares Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo,wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Mary Natema akiwanywesha  juisi baadhi ya watoto yatima waliohudhulia uzinduzi wa kampeni ya Share and Care.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusioano wa Vodacom Tanzania akiongea jambo na Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Stela Chiwango pamoja na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule

Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation”Yessaya Mwakifulefule akitwishwa kiroba cha Maharage na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa kampuni hiyo Matina Nkurlu kushoto na Meneja wa akaunti na usajili wa namba za simu Loius Maro

Meneja wa kitengo cha m pesa kanda ya pwani wa Vodacom Tanzania Nabwike Kibona akimtayarishia chai Ramadhani Abdalah ambae ni mtoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre cha Vingunguti

Meneja wa kitengo cha m pesa kanda ya pwani wa Vodacom Tanzania Nabwike Kibona akiwahudumia watoto  yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre cha Vingunguti

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwahudumia chakula baadhi ya watoto  yatima wa vituo mbalimbalivya jijini Dares Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care.

Mtoto yatima wa kituo cha T.H.M.H cha Magomeni jijini Dare Salaam Rebeca Elias akiwa ameshikilia mbuzi mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Stela Chiwango aliemshika begani na Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba watatu toka kulia

No comments: