To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Wednesday, January 4, 2012

Hamad Rashid Afukuzwa CUF


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 

Baraza kuu la uongozi la taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) linaloendelea na kikao chake cha siku moja katika hoteli ya MAZSONS mjini Zanzibar limepokea tuhuma zinzowakabili viongozi na wanachama 14 wa chama kutoka kamati ya utendaji ya taifa.

Hadi saa 9 jioni leo lilisikiliza tuhuma za watano kati ya watuhumiwa ambao ni, 1.HAMAD RASHID MOHAMED(MBUNGE WA WAWI NA MJUMBE WA BARAZA KUU LA UONGOZI CUF TAIFA) 2. DOYO HASSAN DOYO(MJUMBE WA BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA - TANGA), 3. SHOKA KHAMIS JUMA, 4. JUMA SAID SANANI, 5. YASINI MROTWA. Baraza kuu liliwasomea tuhuma zao watano hawa na kuwapa nafasi ya kujitetea kwa sababu wao ni viongozi wa baraza kuu(viongozi wa kitaifa wa chama) kutokana na kifungu cha 10 (5) cha katiba ya chama.

Baada ya kutafakari kwa kina maelezo ya tuhuma zao na utetezi walioutoa, baraza kuu la uongozi la taifa limeridhika kwamba wanne kati yao wamefanya vitendo vinavyowapotezea sifa za kuendelea kuwa wanachama. Hivyo basi, baraza kuu la uongozi la taifa limeamua kuwafukuza uanachama wa CUF viongozi hao wanne ambao ni HAMAD RASHID MOHAMED, DOYO HASSAN DOYO, SHOKA HAMIS JUMA na JUMA SAIDI SANANI. Uamuzi wa baraza kuu la uongozi la taifa kuwafukuza umefanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63 (1) (j), kifungu cha 64 (4), 64 (5), 64 (6) vya katiba ya chama.

Katika kufikia maamuzi hayo, baraza kuu la uongozi la taifa pia lilizingatia matakwa ya kifungu cha 62 (4), 62 (5), na 59 (8) (d) vya katiba ya chama ambavyo vinataka uamuzi wa kuwafukuza uanachama viongozi wa kitaifa wa Chama uwe ume umeungwa mkono na zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa baraza kuu kutoka tanzania bara na zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa baraza kuu wanaotoka zanzibar.
Uamuzi wa kuwafukuza uanachama viongozi hao wanne umeungwa mkono na wajumbe 23 kati ya 25 wa tanzania bara na wajumbe wote 22 wa zanzibar. Wajumbe 2 wa tanzania bara hawakukubaliana na uamuzi huo.
 
Kwa upande wa Yasin Mrotwa, Baraza kuu la uongozi la taifa liliamua kumpa karipio kali kwa mujibu wa kifungu cha 64 (5), (b) huku mwenendo wake ukiendelea kuchunguzwa kati ya kikao hiki na kikao kijacho cha baraza kuu la uongozi la taifa.
Hadi sasa, baraza kuu la uongozi la taifa linaendelea kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama wengine 9 waliobaki. Taarifa ya maamuzi kuwahusu wao itatolewa baada ya kumalizika kikao leo. ''HAKI SAWA KWA WOTE''
Imetolewa na; JULIUS MTATIRO NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA), 04 JANUARI 2012.

No comments: