Rais Jakaya Kikwete leo amefunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Mkoani Iringa. Pamoja na kuhutubia katika kilele hicho pia Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma za maji na wadau mbalimbali wa maji nchini. Pichani ni Rais Kikwete akiwa katika banda la Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo ya mwaka huu yaliyofanyika uwanja wa Samora Mjini Iringa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Meneja Uwajibikaji na Miradi Endelevu wa SBL, Nandi Mwiyombela. |
No comments:
Post a Comment