To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Thursday, April 5, 2012

Chadema yanyang’anywa Ubunge Arusha Mjini

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema

HABARI ambazo zimetufikia hivi punde kutoka Mjini Arusha ni kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imeipoka Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kutoka hukumu ya kesi ya kupinga matokeo iliyofumguliwa na baadhi ya wanachama wa CCM.
Taarifa zinasema Mahakama imeridhika na ushahidi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Godbless Lema alikiuka maadili ya uchaguzi ikiwemo kutoa maneno ya udhalilishaji mgombea wa CCM, hivyo imetengua ubunge wake rasmi.

Taarifa zinasema tayari Godbless Lema amesema atawashauri viongozi wa Juu wa Chedema kukubaliana na matokeo ya utenguzi ili uchaguzi urudiwe, kwani anahakika atashinda kihalali kama ilivyokuwa awali.
Mwandishi wa mtandao huu bado yupo eneo la tukio anaendelea kukusanya taarifa, na inasemekana Lemma anataka kuzungumza na wanahabari rasmi juu ya utenguzi wa mahakama, hivyo muda si mrefu tutawajuza zaidi taarifa nzima.

No comments: