Mabasi hiyo yakiwa yamegongana mbele ni basi la Super Feo na nyuma ni basi la Abood lililokuwa likielekea Mbeya. Ajali hiyo imetokea jana katika eneo la Nyororo, kwenye mteremko yalikuwa yameongozana mabasi mawili ambayo ni Super Feo linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam Songea huku nyuma basi la Abood likifuata kwa kasi ya ajabu.
Wakati dereva wa basi la Super Feo akijaribu kulipita roli lililokuwa mbele yake likielekea Mbeya ghafla mbele yake, aliona kuna roli lingine lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es salaam likiwa limeharibika barabarani, hivyo ikabidi achukue tahadhari ya kusimama ghafla.
Wakati akisimama tayari basi la Abood lilikuwa limeshamfikia na kushindwa kusimama kutokana na mwendo wa kasi hivyo likaligonga basi la Super Feo kwa nyuma, na kujeruhi watu kadhaa akiwemo Dereva huyo ambaye alibanwa na usukani |
No comments:
Post a Comment