Maofisa wa usalama wa Taifa wakiwa wamemnyang'anya kamera na kumtoa eneo lake la kazi Mpigapicha wa magazeti ya The Guardian na Nipashe, Khalfan Said wakati wa ujio wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana.
Maofisa hao wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wapigapicha za habari kufaya kazi zao kwa uhuru jambo linalosababisha kero kwa wapigapicha nchini na hata wakati mwingine kufikia kuwanyang'anya vitendea kazi vyao, kupigwa. Vitendo kama hivi pia vimekuwa vikifanywa na Polisi jambo ambalo linaleta taswira kuwa Wapigapicha nchini ndio watu hatari zaidi kwa vyombo hivi viwili vya usalama. |
No comments:
Post a Comment