WATAHINIWA 67,941 katika Mkoa wa Dar es Salaam wameanza kufanya mtihani wa kidato cha nne jana katika hali ya amani na utulivu.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard Makali alisema watahiniwa wa shule waliojiandikisha ni 38,670 na wa kujitegemea ni 20,313.
Watahiniwa 9,058 walijiandikisha kufanya mtihani wa maarifa (QT).
Katika shule za sekondari ambazo mwandishi alitembelea, alishuhudia wakiendelea na mtihani huku usalama ukiwa umeimarishwa kwa kuwepo askari Polisi.
Miongoni mwa shule zilizotembelewa ni pamoja na Loyola, Makurumla, Jitegemee, Jangwani
na Kibasila zote za jijini Dar es Salaam.
Ofisa Elimu Mkoa, Makali alithibitisha kuwepo hali ya amani na utulivu katika shule zote mkoani hapa.
Alizipongeza pia shule zote pamoja na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa kufanikisha maandalizi ya mtihani huo unaotarajiwa kumalizika wiki ijayo.
“Tangu asubuhi tupo katika pilikapilika za kuvitembelea vituo vya mtihani, tunashukuru kuwa hali ni shwari kwa kuwa hakuna tatizo lolote ambalo limeripotiwa kutokea hadi hivi sasa,” alisema Makali.
Idadi hiyo ya watahiniwa 67,941 wa Dar es Salaam, ni sehemu ya watahiniwa 480,079 nchi nzima.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Necta, John Nchimbi, watahiniwa wa shule nchini jumla ni 349,578 ambao kati yao wasichana ni 150,461 na wavulana ni 199,117.
Watahiniwa wa kujitegemea ni 101, 005 huku wasichana wakiwa 51,464 na wavulana 49,541.
Kwa upande wa watahiniwa wa Maarifa jumla yao ni 29,496 ambao kati yao wasichana ni 18,040 na wavulana ni 11,456.
Ofisa Habari na Mawasiliano huyo alisema mkoani Dar es Salaam hapakuwa na taarifa zozote
za udanganyifu katika mtihani.

No comments:
Post a Comment