To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560                                                 To Advertise on this Blog please Call: O713 397 767 or 0785 555 560
Mail Me

Tuesday, November 22, 2011

Ajali Yaua Wawili Babati

Watu zaidi ya wawili wanahofiwa kufa katika ajali ya gari iliyotokea usiku majira ya saa 6 katika eneo la kijiji cha Mdori Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo watu wawili walionekana miili yao ikiwa imeungua na moto. Ajali hiyo ililihusisha roli la mizigo lililokuwa limetokea Arusha na Fuso lililokuwa limetokea Singida.

Walioteketea kwa moto inadhaniwa kuwa ni dereva na tandiboy waFuso ambao walibanwa katika gari hilo baada ya kukatika cabin.
 Mafuta ya kupikia ya alizeti yalitapakaa katika eneo hilo.
Fuso ilivyoteketea kabisa na moto.
Wanawake wa Kijiji cha Kadori wakichota mafuta yaliyomwagika katika ajali hiyo.Lakini je mafuta haya yaliyomwagika chini ni safi na salama kwa afya.

No comments: